Mkuu wa Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi, Mwanza anapenda kuwajulisha wafuatao kuwa
wamechaguliwa kujiunga na kozi ya Astashahada ya Awali ya Usimamizi wa Wanyamapori na Hima Sheria
(BTCWLE) na Astashahada ya Usimamizi wa Wanyamapori na Hima Sheria (TCWLE) kwa mwaka wa masomo
2020/2021.

MAHAFALI YA 55 YA KOZI ZA BTCWLE 55 na TCWLE 11″

Kwa niaba ya Bodi ya Ushauri ya Chuo na Menejimenti napenda kutumia fursa hii kumshukuru Mhe Mgeni Rasmi Katibu Mkuu Wizara Maliasili na Utalii na Viongozi wote waliojumuika nasi katika mahafali namba 55 na miaka 54 ya Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi kwa Mwaka wa masomo 2019/2020. Mahafali imefanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 12/09/2020. Tunawashukuru sana. Mungu awabariki na kuwasimamia katika utendaji wenu wa majukumu ya kila siku”. Mkuu wa Chuo Pasiansi, Lowaeli Damalu.

“Guard of Honor” wakiwa wamejipanga kwenye gwaride la heshima kumsubiri mgeni rasmi
Mh. Dkt, Aloyce K. Nziku akiwasili na kupokelewa na Mkuu wa Taasisi kwa ajili ya kukagua Gwaride la Heshima wakati wa Sherehe za Mahafali ya 55 ya Taasisi.
Mh. Katibu Mkuu akisalimiana na baadhi ya wageni waliowasili kwa ajili ya Sherehe za Mahafali ya 55 ya kozi za BTCWLE na TCWLE
Mh. Mgeni rasmi akipanda mti kwenye eneo la
Taasisi kama kielelezo cha utunzaji mazingira
Gwaride la wahitimu wa kozi za BTCWLE 55 na TCWLE 11, Tarehe 12 Sept, 2020

Ziara ya Mhe. Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt Aloyce Nziku katika Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi. Ndugu Viongozi Wakuu wa Taasisi, Mashirika, Idara na Vitengo  napenda kuwafahamisha kwa kifupi kuwa Tarehe 7/8/2020 Chuo kilipata bahati ya kutembelewa na Katibu Mkuu Wizara Maliasili na Utalii kama picha husika zinavyojieleza. Tunakushuru sana Katibu Mkuu kwa kufanya Ziara husika . Tumefaidika mengi kuhusu ujio wako na tuna ahidi kutekeleza maelekezo mapya yote ya kazi uliyoyatoa

  1. CHUO CHA TAALUMA YA WANYAMAPORI – PASIANSI-MWANZA KINAPENDA KUWATANGAZIA WANACHUO KOZI ZA BTCWLE NO. 55 NA TCWLE NO. 11 KWA MWAKA 2019/2020 KUWA WANATAKIWA KUFIKA CHUO TAREHE 30/05/2020 SAA 1:00 ASUBUHI TAYARI KWENDA KAMBI YA MAFUNZO FORT IKOMA WILAYA YA SERENGETI. KUENDELEA NA MAFUNZO KWA VITENDO YATAKAYOANZA TAREHE 01 JUNI 2020.
  • AIDHA, KWA WALE WANAOTOKEA MAENEO AMBAYO USAFIRI WAKE UNAFIKA/UNAPITA FORT IKOMA, WANASHAURIWA KURIPOTI MOJA KWA MOJA KAMBINI FORT IKOMA TAREHE 30/05/2020. USAFIRI WA CHUO KUWAPOKEA KUTOKA KITUO CHA BASI (FORT IKOMA MADUKANI) HADI KAMBI YA MAFUNZO UTAKUWEPO KUANZIA SAA 3:00 ASUBUHI NA SAA 9:00 MCHANA
  • MIZIGO YA WANACHUO ILIYOBAKI CHUONI PASIANSI MWANZA YOTE ITAPELEKWA FORT IKOMA TAREHE 30 MEI 2020.
  • TAHADHARI  ZA KUZUIA MAAMBUKIZI YA UGONJWA COVID-19 IKIWA NI PAMOJA NA KUWAPIMA JOTO LA MWILI KABLA YA KUPOKELEWA CHUO, KILA SIKU ASUBUHI NA JIONI YATAZINGATIWA KAMA ILIVYOELEKEZWA NA SERIKALI. AIDHA,WANACHUO WOTE WAFIKE NA VIFAA VIFUATAVYO:
    • RISTI HALISI YA MALIPO YA ADA
    • BARAKOA ZA KUTOSHA
    • VITAKASA MIKONO BINAFSI (SANITIZER)

MKUU WA CHUO

CHUO CHA TAALUMA YA WANYAMAPORI PASIANSI – MWANZA

Mkuu wa Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi, Mwanza anapenda kuwajulisha wafuatao kuwa
wamechaguliwa kujiunga na kozi ya Astashahada ya Awali ya Usimamizi wa Wanyamapori na Hima Sheria
(BTCWLE) na Astashahada ya Usimamizi wa Wanyamapori na Hima Sheria (TCWLE) kwa mwaka wa masomo
2019/2020. Waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti kuanzia tarehe 16 hadi 18 Septemba 2019 kwa mafunzo ya awali ya
kupima utimamu wa mwili na afya.

The Institute offers two courses, Basic Technician Certificate in Wildlife Management and Law Enforcement and Technician Certificate in Wildlife Management and Law Enforcement, the course duration is 1 year for each course.

Key stakeholders’ Curriculum Development and Review validation workshop on 8th-9th july 2019