Sekretarieti ya ajira yatangaza nafasi za kazi zaidi ya 1,000.

Serikali kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia watanzania wenye sifa na uwezo kujaza jumla ya nafasi wazi za kazi 1,101.
Nafasi hizi za kazi ni kwa ajili ya Katibu mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii na Mtendaji Mkuu Wakala wa Misitu Tanzania (TFS).
Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi nafasi hizo za kazi ambazo zimetangazwa tarehe 9 Julai, 2015 zinapatikana kwenye Recruitment Portal ya Sekretarieti ya ajira kwa kufungua portal.ajira.go.tz ambapo waombaji kazi wote kwa nafasi hizo wanatakiwa kutuma maombi yao ya kazi kwa kutumia mfumo huo.

Ingia kwenye anuani hii ya www.ajira.go.tz upande wa kushoto utaona tangazo kisha lidownload na ufuate maelekezo ya namna ya kuapply.