SHINDANO LA KUANDAA NEMBO (LOGO) KWA AJILI YA MIAKA 50 YA TAASISI

TAASISI YA TAALUMA YA WANYAMAPORI -PASIANSI
CHUO CHA TAALUMA YA WANYAMAPORI
PASIANSI-MWANZA
SHINDANO LA KUANDAA NEMBO (LOGO) KWA AJILI YA MIAKA 50 YA TAASISI
Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi inayo furaha kuyatangazia makampuni yote
yaliyosajiliwa pamoja na watu binafsi wenye uzoefu wa kutengeneza nembo (Logo) kuingia
katika shindano la kutengeneza nembo (Logo) kwa ajili ya miaka 50 ya Taasisi. Uzinduzi wa
maandalizi hayo utafanyika wakati wa mahafali ya miaka 50 ya Taasisi, tarehe 13 Juni, 2015, na
maadhimisho rasmi yatafanyika mwezi Juni, 2016 sambamba na mahafali ya 51 ya Taasisi.
DIRA YA TAASISI: Kuwa kitovu cha ufanisi katika kutoa mafunzo stahili ya Hima Sheria kwa
ajili ya usimamizi endelevu wa wanyamapori.
DHIMA YA TAASISI: Kuzalisha askari wanyamapori bora watakaoweza kulinda raslimali ya
wanyamapori, kupitia mafunzo ya kijeshi, usimamizi wanyamapori, hima sheria na ulinzi pamoja
na huduma za utafiti.
Vigezo vifuatavyo vitatakiwa kuzingatiwa katika uandaaji wa nembo (Logo) hiyo:
Majukumu ya Taasisi, kutimiza miaka hamsini (50) ya Taasisi, rangi ya Taasisi iwe ya kijani,
njano (light yellow), Nembo (Logo) iwe inasomeka vizuri, kubuni kauli mbiu ya maadhimisho
ya miaka 50 ya Taasisi kwa kuzingatia dira na dhima ya Taasisi. Mshindi katika shindano hilo,
atajishindia kiasi cha fedha taslimu (TZS) milioni mbili (2,000,000/=). Washiriki wote
watatakiwa kuwasilisha nembo (Logo) watakazoandaa kabla ya tarehe 05/03/2015. Watumishi
wa Taasisi hawaruhusiwi kushiriki katika shindano hili.
Taasisi inawatakia ushiriki mzuri katika shindano hili.
KWA TAARIFA ZAIDI WASILIANA NA:
Mkuu wa Taasisi,
Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori – Pasiansi,
S. L. P 1432,
MWANZA.
Nukshi: +255-(0) 28-2560333 au +255-(0) 28-2561173/4
Simu ya Ofisini: +255-(0)28-2560333 or +255-(0)28-2561173/4
Simu ya Mkononi: +255 758 255 930
Tovuti: htpp://www.pasiansiwildlife.ac.tz
Barua Pepe: principal@pasiansiwildlife.ac.tz

Leave a Reply

*