27
MAY
2020

TANGAZO KWA WANACHUO MWAKA WA MASOMO 2019/2020

  1. CHUO CHA TAALUMA YA WANYAMAPORI – PASIANSI-MWANZA KINAPENDA KUWATANGAZIA WANACHUO KOZI ZA BTCWLE NO. 55 NA TCWLE NO. 11 KWA MWAKA 2019/2020 KUWA WANATAKIWA KUFIKA CHUO TAREHE 30/05/2020 SAA 1:00 ASUBUHI TAYARI KWENDA KAMBI YA MAFUNZO FORT IKOMA WILAYA YA SERENGETI. KUENDELEA NA MAFUNZO KWA VITENDO YATAKAYOANZA TAREHE 01 JUNI 2020.
  • AIDHA, KWA WALE WANAOTOKEA MAENEO AMBAYO USAFIRI WAKE UNAFIKA/UNAPITA FORT IKOMA, WANASHAURIWA KURIPOTI MOJA KWA MOJA KAMBINI FORT IKOMA TAREHE 30/05/2020. USAFIRI WA CHUO KUWAPOKEA KUTOKA KITUO CHA BASI (FORT IKOMA MADUKANI) HADI KAMBI YA MAFUNZO UTAKUWEPO KUANZIA SAA 3:00 ASUBUHI NA SAA 9:00 MCHANA
  • MIZIGO YA WANACHUO ILIYOBAKI CHUONI PASIANSI MWANZA YOTE ITAPELEKWA FORT IKOMA TAREHE 30 MEI 2020.
  • TAHADHARI  ZA KUZUIA MAAMBUKIZI YA UGONJWA COVID-19 IKIWA NI PAMOJA NA KUWAPIMA JOTO LA MWILI KABLA YA KUPOKELEWA CHUO, KILA SIKU ASUBUHI NA JIONI YATAZINGATIWA KAMA ILIVYOELEKEZWA NA SERIKALI. AIDHA,WANACHUO WOTE WAFIKE NA VIFAA VIFUATAVYO:
    • RISTI HALISI YA MALIPO YA ADA
    • BARAKOA ZA KUTOSHA
    • VITAKASA MIKONO BINAFSI (SANITIZER)

MKUU WA CHUO

CHUO CHA TAALUMA YA WANYAMAPORI PASIANSI – MWANZA