14
SEP
2020

MAHAFALI YA 55 YA KOZI ZA BTCWLE 55 na TCWLE 11

MAHAFALI YA 55 YA KOZI ZA BTCWLE 55 na TCWLE 11″

Kwa niaba ya Bodi ya Ushauri ya Chuo na Menejimenti napenda kutumia fursa hii kumshukuru Mhe Mgeni Rasmi Katibu Mkuu Wizara Maliasili na Utalii na Viongozi wote waliojumuika nasi katika mahafali namba 55 na miaka 54 ya Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi kwa Mwaka wa masomo 2019/2020. Mahafali imefanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 12/09/2020. Tunawashukuru sana. Mungu awabariki na kuwasimamia katika utendaji wenu wa majukumu ya kila siku”. Mkuu wa Chuo Pasiansi, Lowaeli Damalu.

“Guard of Honor” wakiwa wamejipanga kwenye gwaride la heshima kumsubiri mgeni rasmi
Mh. Dkt, Aloyce K. Nziku akiwasili na kupokelewa na Mkuu wa Taasisi kwa ajili ya kukagua Gwaride la Heshima wakati wa Sherehe za Mahafali ya 55 ya Taasisi.
Mh. Katibu Mkuu akisalimiana na baadhi ya wageni waliowasili kwa ajili ya Sherehe za Mahafali ya 55 ya kozi za BTCWLE na TCWLE
Mh. Mgeni rasmi akipanda mti kwenye eneo la
Taasisi kama kielelezo cha utunzaji mazingira
Gwaride la wahitimu wa kozi za BTCWLE 55 na TCWLE 11, Tarehe 12 Sept, 2020