JUMA LA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 TOKA TAASISI TAALUMA YA WANYAMAPORI IANZISHWE (1966-2016)

Mhe. Mkuu wa Mkoa Bw. John Mongella leo tarehe 9/6/2016 amezindua rasmi juma la maonyesho ya shughuli za Taasisi.

Maonyesho haya yataendelea mpaka tarehe 15/6/2016, Wananchi wote mnakaribishwa kuja kujionea shughuli mbalimbali zifanywazo na Taasisi hii ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi. Kauli mbiu ya Maonyesho haya ni uhifadhi endelevu wa Wanyamapori kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.