Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi

Habari
TANGAZO LA MAOMBI YA KAZI YA ASKARI ULINZI KATIKA KAMPUNI YA ULINZI YA PASIANSI (PASCO) 10/07/2023

TANGAZO LA KAZI ZA ULINZI


Mkurugenzi wa Kampuni ya Ulinzi ya Pasiansi Wildlife Security Company Limited (PASCO) anatangaza nafasi 100 za askari ulinzi kwa wahitimu waliomaliza katika Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori-Pasiansi katika kozi za Astashahada na Astashahada ya Awali ya Uhifadhi Wanyamapori au Waongoza Wageni.


Sifa za waombaji
i) Amehitimu mafunzo ya mwaka mmoja yanayotolewa na Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori-Pasiansi katika ngazi ya astashahada ya awali na astashahada
ii) Awe na umri wa miaka 25 na kuendelea
iii) Amehitimu kidato cha nne na kuendelea.
iv) Awe na cheti cha kuzaliwa.
v) Awe na kitambulisho cha NIDA
vi) Awe na Bima ya afya [NHIF];
vii) Awe na TIN namba.


Maombi yatumwe kwa: -


Mkurugenzi,
Pasiansi Wildlife Security Company Limited,
S.L.P 1432,
MWANZA.
Email: principal@pasiansiwildlife.ac.tz


Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 22/07/2023.

 

BONYEZA HAPA KUPATA TANGAZO LA MAOMBI YA KAZI ZA ASKARI ULINZI PASCO 10 JULAI 2023