Habari
TANGAZO LA MAOMBI YA KAZI YA ULINZI KATIKA KAMPUNI YA ULINZI YA PASIANSI (PASCO) 09/06/2023
TANGAZO LA KAZI ZA ULINZI
Mkurugenzi wa Kampuni ya Ulinzi ya Pasiansi Wildlife Security Company Limited (PASCO) anatangaza nafasi za ulinzi kwa wahitimu waliomaliza katika Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori-Pasiansi.
Sifa za waombaji
i) Amehitimu mafunzo ya mwaka mmoja yanayotolewa na Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori-Pasiansi katika ngazi ya astashahada ya awali na astashahada
ii) Awe na umri wa miaka 25 na kuendelea
iii) Amehitimu kidato cha nne na kuendelea.
iv) Awe na cheti cha kuzaliwa.
v) Awe na kitambulisho cha NIDA
vi) Awe na Bima ya afya [NHIF];
vii) Awe na TIN namba.
Maombi yatumwe kwa: -
Mkurugenzi,
Pasiansi Wildlife Security Company Limited,
S.L.P 1432,
MWANZA.
Email: principal@pasiansiwildlife.ac.tz
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 20/06/2023.